Hakika hamna
tanzu ya fasihi iliyo bora kuliko nyingine. Kama vile jazanda ya mti
ilivyoonyesha. Tanzu zote tatu zinatoshana barabara kwa hadhi ya kuakilisha
fasihi. Iwe
(i) Andishi
(matawi): inayokumbatia riwaya, tamthilia na diwani;
(ii)
Simulizi (majani): inayokumbatia tamba, kukariri, kuimba na mijadala; au
(iii)
Onyeshi (maua): inayokumbatia uigizaji, tamasha kama vile denzi na mieleka na
sinema.
Tunapotaka
kutathmini ubora wa fasihi vipo vigezo vinavyotumika ambavyo hutangulia na
kutofautisha fasihi katika sehemu mbili maarufu: (a) fasihi dhati na (b) fasihi
pendwa