Lorenzo: Che meingia, usiku achekelewa
           Kwa miale yake mawingu azikata
           Na kutawanya giza aliyezagaa
           Kama mayungi majini yanavyolewa
           Jua laoneka wazi. Litazunguka
           Falaki yake likiangaza mimea.
           Lilo jicho lake Mungu huchemsha anga
           Hapa bustani lazima nipande tuka
           Mama ardhi ni mwenye miujiza kweli.
           Mji mwake ndimo tukifa huzikwa sisi
           Na huzalishwa dhuria mwake tumboni
           Ambao huwa mlo aina anuwai
           Kwa viumbe vyote vilio na uhai.
           Alamina kujaza dunia arzaki
           Majaza yasiyokuwa nacho kifani
           Alhasili: miti, mawe nazo madini
           Yote chimbuko yao ni ardhini hapa
           Walakini shida huwa yeye ingawa
           Huzingatia kuleta yaliyo mema.
           Wengine nao huyatumia vibaya.
           Ila, isipokuwa kwa nahusi. Badala
           Insafu nuiwa. Patukia ukuba
           Usio wa kutazamiwa. Mfano mmoja
           Ni hili ua: Ni sumu tena ni dawa.
           Ukililamba unakufa wako mwili
           Kilinusa, unachechemka wote mwili.
           Zimefanywa zote hizo mardufu kazi
           Kwa kutumiwa kitu kimoja tu hiki.
           Hivyo hata binadamu tulivyo nafsi
           Tuna hisani pamoja na uhasidi
           Maulana basi ubaya yetu ndani
           Sije tawala juu yake hasanati.